Mtandao wa Wanawake Watoa Tamko Kuhusu Miswada ya Uchaguzi
By WFT-T
01 February 2024
Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uchaguzi na Uongozi jana tarehe 22/1/2024 walitoa tamko lao kuhusu miswada mitatu iliyowasilishwa Bungeni hivi karibuni.
Katika tamko lao, wanamtandao hao wameitaka kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhakikisha suala la misingi ya usawa wa kijinsia linawekwa katika miswada hiyo. Miswada hiyo ni pamoja na Mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani,2023, Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, 2023 na Mswada wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, 2023.
Wakiwasilisha maoni yao mbele ya vyombo vya habari, wanamtandao hao walisema baada ya kufanya uchambuzi yakinifu wa miswada yote mitatu wamegundua uwepo wa mapengo ya Jinsia katika miswada hiyo.
“Tamko hili linahusu madai yetu kwamba nchi yetu inatakiwa iwe na sheria zenye kubainisha usawa wa jinsia pamoja na kuanisha misingi ya uwajibishwaji kwa wale wote wanaopewa dhamana ya uongozi katika kutafsiri misingi hii katika sera na mipango mikakati ya utekelezwaji”Alisema Mary Ndaro, Kaimu Mwenyekiti wa mtandao.
Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uchaguzi na Uongozi unaojumisha mitandao, mashirika na asasi za kiraia takribani 200.
Kupata maelezo kwa undani kuhusu maoni ya Mtandao bofya hapa kusoma Tamko hili
https://ipf- website.s3.euwest3.amazonaws.com/TAMKO_LA_MTANDAO_WA_WANAWAKE_KUHUSU_MISWADA_INAYOHUSIANA_NA_UCHAGUZI_1affada8fd.pdf