Move With Us:

619F9251.JPG
cover image for SUPPORT FEMINIST MOVEMENTS IN UKRAINE, POLAND, and BULGARIA NOW blog
Share

Wanamtandao Watafakari Ushiriki wa Wanawake Katika Michakato ya Demokrasia

By WFT-T

24 May 2024

Katika kuendeleza ajenda ya Katiba yenye mrengo wa jinsia nchi Tanzania, Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uchaguzi na Uongozi umefanya kongamano la kitaifa Tarehe 20-21 Mei jijini Dar-es-salaam ililojumuisha wanamtandao zaidi ya 200 kuotka katika mikoa mbalimbali. Lengo kuu la Kongamano hilo lilikua ni kutafakari na kupanga mikakati ya ushiriki mpana na wenye tija wa wanawake katika kuendelea kuongoza harakati za kuchagiza demokrasia shirikishi.

Kauli Mbiu ya kongamono hili ilikua ni Ajenda Ya Mwanamke; Turufu Ya Ushindi

Akitoa salamu za ufunguzi katika kongamano hilo, mweyenkiti wa Mtando huo Prof .Penina Mlama , amesema matumaini makubwa ya kongamano hilo ni kutoka na mikakati wezeshi iliyojikita katika kuimarisha Mtandao na tapo kwa ujumla katika umiliki wa pamoja wa ajenda;utetezi na ushawishi wa ajenda katika muktadha mzima wa demokrasia shirikishi kwenye ngazi mbalimbali kwa kipindi chote cha uchaguzi na kuendelea.

“kongangamano hili linatoa uwanda mpana wa majadiliano, tafakari na kujikumbusha kuhusu umuhimu wa nguvu ya pamoja, kubainisha mapungufu na mafanikio yaliyojitokeza yanayotokana na jitihada za nguvu za pamoja katika kuhakikisha kuwa sauti za wanawake wote hususan walio pembezoni zinajitokeza na kusikika kwa wingi katika mwendelezo wa kupigania ajenda ya ukombozi wa mwanamke kimapinduzi hususan tunapoelekea katika chaguzi muhimu za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu”

Alisisitiza kwamba takwimu za za hali ya ushiriki wa wanawake kwenye ngazi zote za uongozi kwa wanawake kisiasa bado upo chini ukilinganisha na wanaume mfano wabunge wakuchaguliwa majimboni wanawake ni 26 kati ya 264, wenyeviti wa Kijiji 2.1%, serikali ya mtaa 12.6% hivyo kjitihada za makusudi bado zinahitajika

Vilevile Prof Penina alitoa wito kwa Wanamtandao wote na Wanawake kwa ujumla kuendelea kushiriki na kujitokeza kwa wingi katika kuendeleza harakati za ukombozi wa mwanamke kufikia rasilimali za kitaifa na kijamii, kushiriki kikamilifu katika maamuzi muhimu ya kitaifa mathalani mchakato wa kutoa maoni kuhusu (Dira ya Maendeleo ya Uchumi wa Taifa 2050) unaoendelea katika kupanga mipango ya pamoja na kuingizwa misingi ya haki za wanawake kwenye muktadha za kiuchumi,kijamii na kisiasa itakayopelekea Maendeleo na Ustawi wa wanawake hapa nchini

Katika kongamano hili walishiriki walipata nafasi ya kutafakari mada mbalimba mbali ikiwemo safari ya mtandao toka ulipoanza, mijadala ya kuangazia nini kifanyike ili kuimarisha mtandao na nguu ya pamoja, uchambuzi wa muktadha, na simulizi za mabadiliko katika harakati.

Mwisho wa kongamano wana mtandao kwa umoja wao walitoa tamko la mtandao lenye madai saba likilenga kuimarisha ushiriki wa wanawake katika michakato ya demokrasia hasa kuelekea chaguzi zijazo

Kusoma Tamko la wanamtandao bonyeza hapa

RECOMMENDED BLOGS

View All
StopWar-8M-1024x1024.jpg

Not Provided

The war in Ukraine is intensifying at an alarming rate, with the Russian invasion leading to massive violations of human rights and international humanitarian law, massive migration, death, violence, and destruction.

January 1, 1970

Read this blog post

STRENGTHENING-THE-SEXUAL-AND-REPRODUCTIVE-HEALTH-RIGHTS-COALITION-e1646642456595-1024x529.jpg

Not Provided

Intersectionality is important in tackling inequalities and injustices towards women, girls, children and other social justice actors so as not to perpetuate inequality in systems

November 18, 2022

Read this blog post

2-1024x683.jpg

Not Provided

We have made history! 2015 in Tanzania was definitely a year of firsts! We saw the inauguration of the first Female Vice President; had women actively observing our general elections for the first time; had the first of its kind monitoring system to minimize any act of sextortion; and the first time that so many women went in vying for electoral positions.

November 18, 2022

Read this blog post